DODOMA-Wanafunzi wa Shule ya Msingi Brother Martin ya mkoani Dodoma wamepata elimu ya vipimo kutoka kwa Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Wakala wa Vipimo (WMA),Bi.Veronica Simba katika Banda la Wakala hiyo lililopo kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika katika Viwanja vya Nanenane Nzuguni jijini Dodoma.
Moja ya mikakati ya WMA katika kupanua wigo wa utoaji elimu ya vipimo ni kuanzisha vilabu (clubs) za vipimo katika shule mbalimbali nchini ili kuwajengea uelewa wanafunzi.


