Dkt.Mwinyi aahidi neema zaidi Pemba,shangwe zatawala huku wapinzani wakirejea CCM

PEMBA-Mgombea Urais Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameahidi hatua madhubuti za kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Kisiwa cha Pemba ikiwa ni sehemu ya ahadi zake katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Akihutubia maelfu ya wananchi wa Pemba katika Viwanja vya Gombani ya Kale, Wilaya ya Chakechake leo Septemba 15,2025, Dkt.Mwinyi ametangaza kuwa, Serikali itakabidhi rasmi mkataba wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba ifikapo Septemba 25, 2025 hatua inayotarajiwa kufungua fursa zaidi za utalii, biashara na ajira.
Katika mkutano huo mkubwa wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt.Mwinyi pia ameeleza mipango ya kuwapatia wananchi wa mashamba ya karafuu hati miliki, ili kuwawezesha kuyamiliki kisheria, kuyatunza, na kuyarithisha kwa vizazi vijavyo.
Pia, ameahidi ujenzi na ukamilishaji wa barabara ya Chake Chake-Mkoani ili kuboresha miundombinu ya usafirishaji kisiwani Pemba.

Vilevile,ujenzi wa nyumba 10,000 za gharama nafuu kwa ajili ya wananchi wa Unguja na Pemba.

Ikiweko kuimarishwa kwa uwekezaji na sekta ya viwanda, sambamba na kuongeza ajira kwa vijana kupitia mazingira bora ya biashara.

ASANTENI SANA PEMBA

✈️ Serikali itakabidhi mkataba wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba ifikapo Septemba 25, hatua itakayofungua fursa zaidi za utalii na uchumi.

🌿 Wananchi wa mashamba ya karafuu watapatiwa hati miliki ili kuyamiliki, kuyatunza na kurithisha vizazi vijavyo.

🛣️ Tutakamilisha barabara ya Chake Chake–Mkoani na kuimarisha mtandao wa usafiri Pemba.

🏠 Serikali ijayo itajenga nyumba 10,000 za gharama nafuu Unguja na Pemba.


📈 Tutaimarisha uwekezaji, viwanda na kuongeza ajira kwa vijana.

"Naomba ridhaa ya Wazanzibari kuendelea kulihudumia Taifa letu kwa amani, mshikamano na mshikikano."

#Mwinyi2025 
#ZanzibarMaendeleo
#UongoziUnaoachaAlama

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news