CHAMA Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) kimeandaa mafunzo yatakayowakutanisha Wafanyakazi na Waajiri yanayojulikana kama “Semina ya Waajiri na Viongozi wa Matawi ya TUGHE yatakayofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 15-18 Septemba 2025.

Mafunzo hayo muhimu yanatarajia kuwakutanisha takribani washiriki 1000 kutoka kutoka Serikalini na Taasisi za Serikali na Binafsi ambapo walengwa wakuu ni pamoja na Wakuu wa Taasisi (Mamlaka za Ajira), Wakuu wa Idara, Viongozi wa Matawi ya TUGHE, Wawakilishi wa Makundi Maalum, Makatibu wa Afya/Matron/MOI/DMO/RMO, Maafisa Ustawi wa Jamii, Wanasheria na Maafisa Uhusiano wa Taasisi, Makatibu na Makatibu Wasaidizi wa Mabaraza ya Wafanyakazi.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo



















.jpeg)