ZANZIBAR-Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar, Ramadhan Bukini na Mkurugenzi Muendeshaji wa PBZ, Fahad Soud wametia saini mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya jumla ya shilingi milioni 550 kwa ajili ya mashindano ya YamleYamle Cup.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, mwaka wa kwanza utahusisha malipo ya shilingi milioni 90, huku kila mwaka yakiongezeka kwa asilimia 10 hadi kukamilisha kipindi cha miaka mitano.
