SONGWE-Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) Mkoa wa Songwe imeokoa zaidi ya shilingi milioni 7 za vifaa vya ujenzi wa Soko la Machinga Tunduma.
Picha na mtandao.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Songwe,Frida Wikesi ambayo imeelezea mafanikio ya taasisi katika kipindi cha Aprili hadi Juni,mwaka huu.
"Mmoja wa wazabuni Bi.Rahabu Lunanilo Mkola alipewa kazi ya kusambaza marumaru yenye jumla ya shilingi 24,813,022.69 fedha ambazo alilipwa zote.Licha ya kulipwa fedha hizo,mzabuni hakuwasilisha kwenye mradi marumaru boksi 165 zenye thamani ya shilingi milioni 7.92."

-01.jpg)
-02.jpg)