Waziri Kombo ampokea Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Hungary

DAR-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo amempokea rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Hungary, Mhe. Péter Szijjártó baada ya kuwasili katika Ofisi Ndogo za Wizara za jijini Dar es Salaam leo Septemba 29, 2025.
Akiwa wizarani hapo, Mhe. Szijjártó amekutana kwa mazungumzo ya faragha na mwenyeji wake Mhe. Balozi Kombo yaliyofuatiwa na mazungumzo ya pande mbili ambayo yaliwashirikisha wajumbe mbalimbali kutoka Tanzania na Hungary wakiwemo mawaziri.
Mhe. Szijjártó yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia baina ya Tanzania na Hungary.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news