Jinsi ya kumpigia kura mgombea Urais wa Zanzibar, Dkt.Hussein Ali Mwinyi kesho,kura nyingi za ndio kwa ustawi bora wa jamii na Taifa

NDUGU wananchi,
kesho tarehe 29 Oktoba 2025, ndiyo siku yetu. Siku tuliyokuwa tukiisubiri kwa hamu, siku ya kutimiza safari ya matumaini, safari ya ahadi, na safari ya maendeleo.
Kupitia Kampeni za CCM tulizofanya katika maeneo mbalimbali ya Unguja na Pemba, tumekutana na makundi tofauti ya wananchi, tumesikiliza changamoto zao, na tumeainisha suluhisho ndani ya Ilani ya CCM 2025–2030.

Katika kila hatua, nimewaahidi Wazanzibari kuendeleza kwa kasi zaidi maendeleo ya kweli na huduma bora. Katika awamu ijayo, dhamira yangu ni kuona Zanzibar inaendelea kusonga mbele kimaendeleo, ikiwa na amani, umoja, na ustawi.
Kesho ni siku ya kufanya maamuzi.

■Tuchague maendeleo.
Tuchague uthabiti.
Tuchague matokeo.Nichagueni mimi, Hussein Ali Mwinyi, kwa kura nyingi za NDIO.

Oktoba Tunatiki kwa CCM ✅ na Dkt. Hussein Ali Mwinyi ✅

#HAM2025 

#UongoziUnaoachaAlama 
#KuraNiAlamaYaMaendeleo

#CCM2025

Imetolewa na mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo Oktoba 28,2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news