Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) wameungana kuimarisha juhudi za kuhakikisha mazingira salama, jumuishi na yenye afya katika vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi nchini Tanzania.
Kuanzia Oktoba 15 hadi 17, 2025, UNESCO iliendesha mafunzo maalum ya kozi ya mtandaoni ihusuyo elimu ya kina ya stadi za maisha zinazozingatia VVU/UKIMWI, Afya ya uzazi na jinsia (CSE), hatua inayolenga kuwawezesha wanafunzi kupata maarifa muhimu kuhusu afya, usalama na ustawi wao katika maisha ya chuoni na baada ya masomo.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mwakilishi Mkazi na Mkuu wa ofisi ya UNESCO Bw. Michel Toto alisema, "Ushirikiano huu unaakisi dira yetu ya pamoja ya kuhakikisha kila mwanafunzi anasoma na kustawi katika mazingira salama bila vikwazo.”
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo

























