KAGERA-Mahakama ya Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera chini ya Hakimu Mfawidhi Mheshimiwa Yohana Muyombo leo Oktoba 17,2025 imemhukumu kifungo cha miaka mitatu jela bila faini mfanyabiashara Martine Muyobya Tabura.
Picha na mtandao.
Ni baada ya kupatikana na hatia ya kushiriki vitendo vya rushwa na kuingiza bidhaa nchini kwa njia za magendo.
Katika kesi ya jinai namba CC 25329/2025, Muyobya alishtakiwa kwa kosa la kukiuka kifungu cha 15(1)(a) na (2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Sura ya 329, Marejeo ya Mwaka 2023.
Mahakama ilielezwa kuwa,kati ya tarehe 11 hadi 25 Julai, 2025, mshtakiwa akiwa mfanyabiashara, aliingiza vifaa vya muziki vyenye thamani ya shilingi 9,285,714 kutoka nchini Uganda kwa njia za magendo bila kulipa kodi stahiki ya serikali.
Kitendo hicho kilisababisha hasara kwa serikali ya jumla ya shilingi 3,958,118 ikiwa ni kodi iliyopaswa kulipwa.
Shauri hilo liliendeshwa na waendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Bw. Sospeter Joseph na Bw. William Musso, ambao waliwasilisha ushahidi uliowezesha Mahakama kutoa hukumu hiyo kali.
Tags
Biashara za Magendo
Breaking News
Habari
Mahakamani Leo
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
TAKUKURU
.jpeg)