NA DIRAMAKINI
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya hali ya hewa kwa wakazi wa maeneo ya pwani na watumiaji wa bahari, ikiwataka kuwa makini na kufuatilia taarifa za hali ya hewa kutokana na kuendelea kusogea kwa Kimbunga CHENGE kuelekea magharibi zaidi mwa Bahari ya Hindi ulipo ukanda wa pwani wa Tanzania.
Hadi kufikia asubuhi ya leo Jumamosi, kimbunga hicho kilikuwa takribani kilomita 1,280 mashariki mwa pwani ya Kisiwa cha Mafia.
Kwa mujibu wa taarifa ya TMA, mfumo huo wa hewa unatarajiwa kupungua nguvu hatua kwa hatua kadri unavyokaribia mwambao wa Tanzania.
TMA imewahimiza wakazi wa maeneo hayo na watumiaji wa bahari kuendelea kufuatilia taarifa na utabiri wa hali ya hewa kila wakati.
Tags
CHENGE Cyclone
Habari
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)
Tanzania Meteorological Agency (TMA)
Utabiri wa Hali ya Hewa Tanzania

