Tume ya Madini yajipanga upya kuboresha Sekta ya Madini nchini

TANGA-Tume ya Madini inaendelea na kikao kazi cha menejimenti jijini Tanga chenye lengo la kutathmini utekelezaji wa majukumu yake na kuweka mikakati mipya ya kuimarisha Sekta ya Madini nchini.
Kupitia kikao hicho, washiriki wanajadili kwa kina njia bora za kuongeza mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa, ikiwemo kuimarisha usimamizi, kuongeza thamani ya madini nchini, na kuhamasisha uwekezaji endelevu katika sekta hiyo.

Tume ya Madini imeendelea kuwa chachu ya maendeleo katika Sekta ya Madini kupitia usimamizi madhubuti, utoaji wa leseni, elimu kwa wachimbaji, na ufuatiliaji wa shughuli za madini katika ngazi zote za uzalishaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news