Watumishi wa umma watakiwa kuzingatia misingi ya uadilifu ili kutoa huduma bora kwa umma

ANTONIA MBWAMBO
NA VERONICA MWAFISI

KATIBU Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi amewakumbusha Watumishi wa Umma kupitia Vyombo mbalimbali vya Habari, kuwajibika katika kutoa huduma Bora kwa Umma kwa kuzingatia Misingi ya Uadilifu ili kuleta Ustawi kwa Wananchi.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akizungumza wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari kuhusu ushiriki wa Watumishi wa Umma katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Mteja uliofanyika katika Ofisi hiyo jijini Dodoma.

Bw. Mkomi ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu ushiriki wa Watumishi wa Umma katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Mteja iliyoanza tarehe 06 hadi 10, Oktoba 2025 yenye Kaulimbiu isemayo “Dhamira Inayowezekana”.

Bw. Mkomi amesema, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ni simamizi katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Mteja, hivyo imeendelea kuzingatia misingi yake ya maadili ikiwemo Uzalendo, Uadilifu, Ubora na Mteja Kwanza ikiwa ni sehemu ya kusimamia Dira ya Ofisi inayofanya kuwa na Utumishi wa Umma wenye ufanisi na uwajibikaji.
Sehemu ya Wakurugenzi wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari kuhusu ushiriki wa Watumishi wa Umma katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Mteja uliofanyika katika Ofisi hiyo jijini Dodoma.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wake na waandishi hao kuhusu ushiriki wa Watumishi wa Umma katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Mteja katika Utumishi wa Umma uliofanyika jijini Dodoma.

Vilevile Katibu Mkuu Mkomi amewataka Watumishi wa Umma kutumia Wiki ya Huduma kwa Mteja kuwa chachu ya mabadiliko katika utendaji kwa kutoa huduma bora na kujenga taswira chanya kwenye ofisi kwa kuzingatia misingi ya maadili ili kupunguza malalamiko na kujenga imani ya wananchi kwa Serikali yao.

Ustawi wa Wananchi utapatikana kupitia utoaji wa huduma bora, unaozingatia maadili ya utendaji na maadili ya taaluma walizonazo Watumishi wa Umma hivyo, wanapotoa huduma wazingatie kuwa nadhifu, waaminifu, wakarimu, wenye heshima, wanaojali utu, kuepuka vitendo vya rushwa na kujali watu wanaowahudumia,” Bw. Mkomi amesisitiza.
Waandishi wa Habari wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma (katikati) mara baada ya Katibu Mkuu huyo kuhitimisha Mkutano wake na Waandishi hao kuhusu ushiriki wa Watumishi wa Umma katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Mteja uliofanyika katika Ofisi hiyo jijini Dodoma.

Katika hatua nyingine alipokuwa akihitimisha hotuba yake, Katibu Mkuu Mkomi amesisitiza Watumishi wa Umma na Wananchi kujitokeza katika Uchaguzi Mkuu wa Serikali utakaofanyika tarehe 29 Oktoba, 2025 ili kutumia haki yao ya Kikatiba ya kuchagua Viongozi watakaoiongoza nchi kwa ustawi wa Taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news