Bodi ya Ligi Kuu Tanzania yatoa onyo kwa Yanga SC na klabu zingine

DAR-Young Africans Sports Club (Yanga SC) imepewa onyo kali kwa kosa la kushindwa kufuata ratiba ya matukio ya mchezo (match countdown) kuelekea mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar Fc uliomalizika kwa Yanga Sc kuibuka na ushindi wa 2-0 kwenye uwanja wa KMC Complex Oktoba 28, 2025, hatua ambayo ni kinyume na matakwa ya Kanuni ya 17:15 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Novemba 11, 2025 na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLP) imeeleza kuwa, Young Africans walishindwa kuwasilisha leseni za wachezaji wao kwa wakati jambo lililochelewesha zoezi la ukaguzi, ambapo ililazimika lifanyike saa 9:44 alasiri badala ya saa 8:50 mchana kama ratiba ilivyoainisha.

Aidha,Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLP) katika kikao chake cha Novemba 11,2025 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya ligi na kufanya maamuzi yafuatayo;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news