Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Godfrey Chongolo (Mb) ameleleza kwa Menejimenti na Watumishi ya Wizara ya Kilimo kuwa kazi na malengo yaliyopangwa yatafikiwa kwa kuendeleza pale Mbunge wa Nzega Mjini, Mhe. Hussein Bashe alipoishia ili kukuza na kuleta tija kwenye Sekta ya Kilimo nchini.
Amempongeza Waziri alyepita Mhe. Bashe, Menejimenti na Watumishi wa Wizara ya Kilimo kwa ujumla kwa kuwa mstari wa mbele katika kubuni miradi mbalimbali ambayo imekuwa ikileta tija na manufaa kwa wakulima na Taifa.Mhe. Waziri Chongolo amesema hayo wakati akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya ofisi na alyekuwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mbunge wa Nzega Mjini),tarehe 18 Novemba 2025, katika Ukumbi wa Wizara, jijini Dodoma.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo





















