TMA yatoa tahadhari ya hali mbaya ya hewa Nyanda za Juu Kusini na Magharibi

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya uwepo wa hali mbaya ya hewa kwa baadhi ya maeneo ya nyanda za juu kusini na magharibi kuanzia Alhamisi, Novemba 20 hadi Jumapili, Novemba 23, 2025.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo leo Novemba 19,2025 imeeleza kuwa, siku ya Alhamisi, Novemba 20,2025 mvua kubwa inatarajiwa kunyesha katika maeneo machache ya mikoa ya Ruvuma na Njombe, hali ambayo huenda ikasababisha athari ikiwemo baadhi ya makazi kuzungukwa na maji.

TMA imeongeza kuwa Ijumaa na Jumamosi ya Novemba 21 hadi 22, mvua kubwa itaendelea katika maeneo machache ya mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe, Iringa, Ruvuma, Morogoro, Singida, Dodoma, Kigoma, Katavi na Tabora.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,athari kuu zinazoweza kujitokeza katika kipindi hicho ni maeneo ya makazi kuathiriwa na maji kutokana na mvua kuongezeka.

Hata hivyo, kwa Novemba 23, TMA imethibitisha kuwa hakuna tahadhari yoyote ya hali mbaya ya hewa iliyotolewa kwa maeneo ya nchi.

Mamlaka hiyo imewataka wananchi wote, hasa wanaoishi maeneo hatarishi, kufuatilia taarifa rasmi zinazotolewa mara kwa mara na kuchukua tahadhari stahiki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here