Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Vision Care ya Korea Kusini imefanikiwa kuwafanyia upasuaji watu 60 waliohitaji huduma ya upasuaji wa mtoto wa jicho kwa njia ya tundu dogo kupitia kambi maalum ya siku tano iliyoanza tarehe 17 Novemba 2025 na kuhitimishwa tarehe Novemba 21, 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhitimisha kambi hiyo Novemba 21, 2025, Mkuu wa Idara ya Macho wa MNH, Dkt. Joachim Kilemile, amesema kuwa kambi hiyo imekuwa na mwitikio mkubwa na imefanikisha kutoa huduma bora kwa wagonjwa waliokuwa wakisubiria kupata huduma hiyo muhimu.
“Takwimu zinaonyesha kuwa mtoto wa jicho ni miongoni mwa changamoto kubwa za kiafya nchini, na husababisha takribani asilimia 20 ya upofu Tanzania. Kati ya wagonjwa 24 wanaofika hospitalini wakiwa vipofu, karibu 19 hupatikana kuwa na tatizo hili, jambo linaloonyesha ukubwa wa hitaji la huduma za matibabu ya mtoto wa jicho,”amesema Dkt. Kilemile.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)










