NA DIRAMAKINI
YOUNG Africans Sports Club (Yanga SC) imejikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Novemba 9,2025.
Nafasi ya pili inashikiliwa na watani zao Simba Sports Club (Simba Simba SC) kwa alama tisa baada ya mechi tatu, huku Yanga ikiwa tayari imecheza mechi nne.
Aidha, Pamba Jiji FC inaendelea kuwa nafasi ya tatu kwa alama tisa baada ya mechi sita, nafasi ya nne inashikiliwa na Mbeya City FC kwa alama nane baada ya mechi sita.
Kwa upande wa nafasi ya tano inashikiliwa na Mashujaa FC kwa alama nane baada ya mechi sita, huku KMC FC ikiburuza mkia kwa alama tatu baada ya mechi sita.
