Taarifa hizi zinazosambazwa X (Twitter) zinalenga uchafuzi wa haiba ya mtu

DAR-Baada ya kufanya uchochezi na kila mbinu za kutaka kuiangusha Serikali iliyopo madarakani, huku wakiambulia patupu, genge la wahalifu linaloongozwa na wanaharakati wenye nia ovu wamekuja na mbinu nyingine za kutaka kupotosha umma.
Kundi hilo limekuja na taarifa zinasambaa katika Mtandao wa X (zamani Twitter) zikidaiwa kumhusisha kijana aliyejitambulisha kwa jina la Abdul Ameir na vitendo vya uvunjifu wa maadili pamoja na matumizi ya lugha zisizofaa.

Taarifa hizo zimekuwa zikisambazwa kwa mfumo wa picha za “screenshot” na baadhi ya watu wanaojiita wanaharakati.

Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa, kusambazwa kwa taarifa hizo kunalenga kupotosha umma na kuichafua Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hasa kutokana na madai ya kuhusishwa kwa Abdul Ameir ambaye ni mtoto wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Wataalamu wa mawasiliano wanasema kuwa, kitendo hicho kinaashiria matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii kwa nia ya kuchafua taswira ya Serikali na viongozi wake.

Taarifa hizo potofu zimeibua mijadala mitandaoni, ambapo wananchi mbalimbali wameendelea kuhoji uhalisia wake huku wakitaka mamlaka husika zichukue hatua dhidi ya wanaosambaza upotoshaji huo.

Aidha,wadau wa habari na mawasiliano wamekemea vikali mienendo hiyo, wakisisitiza kuwa mitandao ya kijamii inapaswa kutumika kwa kujenga taifa, si kubomoa.

Kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Mtandaoni ya mwaka 2015, ni kosa kusambaza taarifa za uongo, za kuchafua au kudhalilisha mtu au taasisi bila uthibitisho.

Pia,wataalamu wanakumbusha kuwa kila raia ana wajibu wa kuhakikisha anachapisha na kusambaza taarifa zenye ukweli na zinazoheshimu misingi ya maadili na utu.

Aidha, Serikali imekuwa ikisisitiza kuwa haitavumilia vitendo vya upotoshaji vinavyolenga kuvuruga amani na umoja wa kitaifa, na imekuwa ikiwataka wananchi kutumia mitandao ya kijamii kwa uwajibikaji na uzalendo ili kuhiletea maendeleo.

Ikumbukwe kuwa, matumizi sahihi ya mitandao ni nguzo muhimu katika kulinda heshima ya taifa, kuimarisha amani, na kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Hivyo,ni jukumu la kila Mtanzania kukemea na kukataa maovu ya upotoshaji, kwani ukweli na maadili ndivyo vinavyoijenga Tanzania tunayoitamani kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Zifuatazo ni baadhi ya taarifa zinazotengenezwa na genge hilo ili kupotosha umma na kutweza utu, tunapaswa kuzipuuza popote pale;


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news