HARARE-Rais wa Zimbabwe, Mheshimiwa Emmerson Mnangagwa amemtumia salamu za pongezi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia ushindi wake mkubwa katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 29,2025.
Katika taarifa yake, Rais Mnangagwa amesema, ushindi wa Rais Samia unaonesha imani na ujasiri wa wananchi wa Tanzania katika uongozi wake pevu na sera za chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Rais Mnangagwa amesisitiza ahadi ya Zimbabwe kuendelea kushirikiana kwa karibu na Tanzania ili kuimarisha na kupanua uhusiano mzuri wa urafiki na mshikamano kati ya mataifa na wananchi wa nchi hizo mbili.
Uchaguzi wa Tanzania ulimalizika hivi karibuni kwa ushindi wa kishindo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).


