DODOMA-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete, amefanya kikao na Watumishi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi za Mamlaka jijini Dodoma.
Katika ziara hiyo iliyofanyika jana Novemba 24, 2025 Waziri Kikwete aliambatana na viongozi wengine akiwemo Naibu Waziri Ofisi ya Rais UTUMISHI Mhe. Regina Qwaray na Katibu Mkuu Ikulu,Bw. Mululi Mahendeka.
Katika kikao hicho pamoja na kukagua shughuli zinazofanywa na mamlaka hio, Waziri Kikwete ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha kuwa mamlaka ina wajibu wa kuendelea kuhakikisha inasimamia na kuendeleza kazi ya kuunganisha serikaki kimtandao na kimifumo huku akisisitiza uwekezaji katika watumishi wa mamlaka ili kuifanya serikali kuendelea kuwa salama kidigitali.
Ziara inaendelea…

