DODOMA-Jumla ya waombaji 14,433 wamechaguliwa kujiunga na mafunzo ya ufundistadi VETA kwa mwaka wa masomo 2026 kati ya 18,875 waliowasilisha maombi.
Kati ya waombaji hao wamo 134 ambao ni wahitimu wa elimu ya juu wenye astashahada, shahada na shahada ya uzamili.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Anthony Kasore, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Desemba 23,2025 amesema,uchaguzi huo umefanyika kwa kuzingatia miongozo na mifumo rasmi ya serikali.
"Jumla ya waombaji 14,433 wamepangiwa kujiunga mafunzo ya ufundi stadi katika vyuo vya VETA kwa ngazi ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2026. Kati yao wanaume ni 8,776 na wanawake ni 5,657.
"Kati ya waliochaguliwa 12,942 wamechaguliwa kwa mafunzo ya asubuhi huku 1,491 wamechaguliwa kwa masomo ya jioni. Waombaji 4,511wanasubiri kupangiwa vyuo vya fani kutokana na kuwa walichagua fani moja tu,"amesema.
