Balozi Kaganda ateta na Mwenyekiti wa Wakuu wa Vyuo vya Ukamanda na Unadhimu Afrika

HARARE-Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. CP Suzan Kaganda amekutana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Wakuu wa Vyuo vya Ukamanda na Unadhimu Afrika (African Conference of Commandants-ACOC),Meja Jenerali Stephen Justice Mnkande.Meja Mnkande ni Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Duluti-Arusha, na anaongoza ujumbe kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ambao upo jijini Harare kuanzia tarehe 01 hadi 05 Disemba, 2025, Zimbabwe kushiriki warsha ya mafunzo ya 17th ya utayari wa Jeshi la Afrika (African Standby Force).

Ni kwa lengo la kuvijengea uwezo vyombo vya ulinzi na usalama kutoka nchi za Umoja wa Afrika (AU) katika kusimamia na kulinda kikamilifu mipaka ya nchi zao na kukabiliana na uhalifu unaohatarisha amani Barani Afrika.
Warsha hiyo pia inatumika kama jukwaa la ukusanyaji michango ya mawazo kutoka kwa nchi washiriki na wadau wengine kuandaa mafunzo ya utayari wa Jeshi la Afrika (African Standby Force) na mapitio ya miongozo ya mafunzo ya kila mwaka kwa vipindi vijavyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here