Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo (aliyesimama katikati) akiwaongoza wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kuimba wimbo wa mshikamano daima wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza hilo uliofanyika Kibaha mkoani Pwani.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo uliofanyika Kibaha mkoani Pwani.
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Bi.Asha Hayeshi akimkaribisha Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo (hayupo pichani) kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo uliofanyika Kibaha mkoani Pwani.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Theresia Mpangala akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 wa Ofisi hiyo wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika Kibaha mkoani Pwani.
Naibu Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali akinadi sera wakati akiomba kura kwa wajumbe wa Baraza hilo ili aweze kuchaguliwa kuwa Katibu wa Baraza wakati wa mkutano wa Baraza hilo uliofanyika Kibaha mkoani Pwani.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakimsikiliza Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano wa Baraza hilo uliofanyika Kibaha mkoani Pwani.Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakichangia mada kuhusu taarifa ya uanzishwaji wa SACCOS ya Ofisi hiyo wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo uliofanyika Kibaha mkoani Pwani.
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Sara Rwezaula akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati wa mkutano wa Baraza hilo uliofanyika Kibaha mkoani Pwani.
Wakili wa Serikali wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, ndugu Hans Mmbando akiwasilisha taarifa ya uanzishwaji wa SACCOS ya Ofisi hiyo wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo uliofanyika Kibaha mkoani.Katibu wa TUGHE Tawi la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, ndugu Festo Nyakunga akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo uliofanyika Kibaha mkoani Pwani.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo (aliyeketi katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa TUGHE Tawi la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kufungua mkutano huo uliofanyika Kibaha mkoni Pwani.
Tags
Habari
Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali
Picha
Picha Chaguo la Mhariri
Wafanyakazi Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali






