MOROGORO-Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro katika kutekeleza majukumu yake ya kuzuia na kutanzua uhalifu limefanya mahojiano na Rasel Mpuya Madaha (49), Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine na mkazi wa Morogoro.
Mahojiano yamefanyika Desemba 2, 2025 na baada ya mahojiano hayo ameruhusiwa kuendelea na shughuli zake wakati uchunguzi zaidi unaendelea kufanyika.
