ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amekutana na wawekezaji pamoja na wamiliki wa makampuni matatu kutoka Jamhuri ya Shirikisho la Brazil yaliyonesha nia ya kuwekeza Zanzibar, katika mazungumzo yaliyofanyika Ikulu, Zanzibar tarehe 16 Desemba 2025.
Makampuni hayo ni Amazon Real Hubs, linalojihusisha na usindikaji na usafirishaji wa korosho pamoja na bidhaa za matunda; West Avest Company, linalojikita katika ufugaji wa kuku na uzalishaji wa mayai; na Trade Hubs Pharmaceutical, linalotoa huduma za tiba pamoja na utengenezaji wa dawa.
Ujumbe wa wawekezaji hao umeongozwa na Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Mheshimiwa Gustavo Martins Noguera, akiambatana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Brazil, Mhe. Dkt. John Stephen Simbachawene.









.jpg)

