Spika Mussa Azzan Zungu akutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya wakiongozwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini

DAR-Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu, amekutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya Mabalozi wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya wakiongozwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Mhe. Christine Grau walipomtembelea leo tarehe 4 Desemba, 2025 katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, walizungumza kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya, ikiwa ni pamoja na kuimarisha diplomasia ya kibunge (Parliamentary Diplomacy).
Kikao hicho kimehudhuria na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania ambao ni Balozi wa Finland, Balozi wa Hispania, Balozi wa Italia, Balozi wa Ubelgiji na Balozi wa Ujerumani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here