Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St.Augustine Mwanza wahimizwa kudumisha amani na kuepuka vitendo vya kihalifu

MWANZA-Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi, DCP Wilbrod Mutafungwa amewahimiza wanafunzi kuepukana na makundi yanayochochea uvunjifu wa amani na badala yake kujikita katika jambo lilowaleta chuoni hapo.
Ameyasema hayo Disemba 6,2025 huko katika Chuo cha ST.Augustine (SAUT) kilichopo Kata ya Luchelele, Wilaya ya Nyamagana, ikiwa ni muendelezo wa kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya kijamii lengo ni kuzuia uhalifu na kuweka mikakati ya pamoja ya kuhakikisha mkoa wa Mwanza unakuwa salama.

Akizungumza katika mkutano huo, Kamanda Mutafungwa, amewataka wanafunzi hao kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutanzua, kutatua pamoja na kutoa taarifa za wahalifu ambao hawana nia nzuri na mkoa wetu iwe chuoni hapo au hata nje ya chuo hicho ili waweze kudhibitiwa kwa haraka na sheria ichukuwe mkondo wake.
Aidha, amewasihi walimu pamoja na wamiliki wa hosteli za wanafunzi kuhakikisha wanaweka ulinzi na usalama wa kutosha kama CCTV kamera hususani katika hosteli za wanafunzi wakike ili kuepukana na matukio ya kihalifu kufanyika katika hosteli hizo

"Usalama ni jukumu la kila Mtanzania, na hivyo kila mmoja anapaswa kuchukua hatua stahiki kulinda eneo lake."
Kwa upande wake Mlezi wa wanafunzi wa chuo hicho Padre Dkt. Japhet Njaule, aliwahimiza wanafunzi kuwa kioo cha jamii kwa kudumisha maadili, kujikita katika masomo na kuendeleza taaluma zao kwani jukumu la mwanafunzi ni kujithamini, kujilinda na kufanya maamuzi yenye tija kwa mustakabali wa maisha yake.
Vilevile, amelishukuru Jeshi la Polisi kuja kutoa elimu kwa wanafunzi hao hususani katika kipindi hiki kigumu ili kuwapa muongozo mwema wa nini wanatakiwa kufanya ili kuepukana na matendo ya uvunjifu wa amani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news