Ukatili wa kijinsia haukubaliki,wanafunzi Mbeya waelezwa

MBEYA-Kuelekea Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limewataka Wanafunzi wa Sekondari kukemea vitendo vya ukatili kwa kutoa taarifa.
Akizungumza Novemba 30, 2025 wakati wa utoaji wa elimu ya kupinga ukatili kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mbeya Day, Mkuu wa Dawati la Jinsia na watoto Mkoa wa Mbeya Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Veronica Ponera amesema kuwa wanaendelea kutoa elimu ya kupinga ukatili ili kupunguza matukio kama vile Kubaka, Kulawiti na vipigo.

Aidha, ASP Ponera ameeleza kuwa bado kuna changamoto ya uwepo wa matukio hayo kuanzia ngazi ya familia na shuleni hivyo amewataka Wanafunzi hao kuwafichua watu wenye tabia hizo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Naye, Mkuu wa Polisi Jamii Wilaya ya Mbeya Mrakibu wa Polisi (SP) Nuru Mahenge amewataka wanafunzi kujiepusha na makundi mabaya na kuacha tamaa ya vitu vidogo vidogo kwani inaweza kuwasababishia madhara makubwa ikiwemo kufanyiwa vitendo vya ukatili.

Kwa upande wake, Mratibu kutoka Shirika lisilo la kiserikali la "CARE INTERNATIONAL" Bi. Mwanane Madebo ameeleza kuwa wamekuwa wakishirikiana na Serikali kuyafikia makundi mbalimbali ya kijamii, Walimu, Wanafunzi, Maafisa Usafirishaji na kutoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili ili kutokomeza vitendo hivyo.
Ameongeza kuwa, Vitendo vya ukatili vinasababisha madhara kwa mhanga, familia na jamii kwa ujumla kwani husababisha vifo, ulemavu na msongo wa mawazo na kuwataka Wanafunzi kutofumbia macho vitendo hivyo na kuwa wepesi kutoa taarifa pindi waonapo viashiria.

Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili 2025 yamebeba kauli mbiu inayosema "Ungana kutokomeza unyanyasaji wa kidijitali dhidi ya Wanawake na Wasichana Wote"

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here