SINGIDA-Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida kupitia Dawati la Jinsia na Watoto, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, limetoa elimu ya matumizi salama ya mitandao kwa wazazi na vijana ili kuwalinda dhidi ya ukatili wa kijinsia wa kidijitali.
Elimu hiyo ilitolewa Novemba 27, 2025, katika Hospitali ya Wilaya ya Singida ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga ukatili wa kijinsia Duniani.
Elimu hiyo ilitolewa Novemba 27, 2025, katika Hospitali ya Wilaya ya Singida ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga ukatili wa kijinsia Duniani.Mkuu wa Dawati la Jinsia ASP Theresia Mdendemi akishirikiana na Inspekta Amina Fakhi waliwaeleza wazazi na vijana namna bora ya kutumia mitandao bila kuingia kwenye hatari, ikiwemo kutowasiliana na watu wasiojulikana, kutambua vitendo vya udhalilishaji na kuweka mipaka ya matumizi ya simu kwa watoto.
Pia walieleza aina za ukatili, athari zake na umuhimu wa kutoa taarifa mapema.
Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Abel Zabroni aliwashukuru kwa elimu hiyo na kuahidi kushirikiana na Jeshi la Polisi kuwaunganisha waathirika wa ukatili na vyombo vya usalama ili kusaidia upatikanaji wa msaada wa kisheria.
Tags
Elimu ya Ukatili wa Kijinsia
Habari
Jeshi la Polisi Tanzania
Matumizi Salama Mitandao
Mitandao ya Kijamii



