Wizara ya Afya yatoa onyo kali kwa wanaotumia jina la Waziri Mohamed Omary Mchengerwa kutapeli watu

DODOMA-Wizara ya Afya imesikitishwa na kitendo cha baadhi ya watu wenye nia ovu ambao wamekuwa wakitumia jina la Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa kuwatapeli watu kwamba anaozesha mwanae, hivyo kuwaomba michango ya harusi ya mtoto wa Mhe. Mchengerwa.
"Tunapenda kutoa taarifa kuwa, Mhe. Mchengerwa hana mtototo anayemuozesha na
kwamba hajawahi kumtuma mtu yoyote kuomba michango kwa ajili ya harusi yoyote.

"Wizara ya Afya inapenda kutoa onyo kwa yoyote anayejihusisha na vitendo hivyo vya uvunjaji wa sheria na kwamba tayari imeshatoa taarifa kwenye mamlaka husika kuhusu namba zote zinazotumika kwa hatua za kisheria.

"Aidha, Wizara inatoa wito kwa viongozi na wananchi wote kwa ujumla kuwapuuza matapeli hao."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news