Jeshi la Polisi lingependa kuwa shukuru wananchi wote kwa ushirikiano mliyoonyesha katika kuupokea na kusheherekea mwaka mpya 2026 kwa amani, utulivu, upendo na usalama.
Kutokana na ushirikiano huo wa kutambua thamani ya kudumisha amani hali ya usalama nchini hadi sasa ni shwari ila kwa masikitiko makubwa tumepoteza Watanzania wenzetu 10 kutokana na ajali ya magari mawili kugongana na kuwaka moto mkoani Morogoro.
Tuna toa wito tuendelee kulinda na kuimarisha amani, utulivu, upendo na usalama wakati wote tunapoendelea kusheherekea mwaka mpya 2026.
Pia tuendelea kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazo zuilika kwa kuwa makini na kuzingatia udereva wa kujihami.
Imetolewa na;
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma,Tanzania
