DODOMA-Benki Kuu ya Tanzania inatoa tahadhari kwa umma kufuatia kuongezeka kwa matangazo na machapisho ya mtandaoni yanayohusisha utapeli wa uwekezaji, yakiwemo yanayotumia picha au video bandia zinazotengenezwa kwa teknolojia ya Akili Unde (AI) na kudai ushiriki wa viongozi wa serikali au watu maarufu.
Wananchi wanahimizwa kuepuka kufungua viungo visivyoeleweka, kutoa taarifa binafsi au kutuma fedha kwa majukwaa yasiyothibitishwa, na kuhakikisha fursa zozote za uwekezaji zinathibitishwa na mamlaka husika kama Benki Kuu ya Tanzania au CMSA, huku matangazo yanayotiliwa shaka yakitakiwa kuripotiwa kwa mamlaka zinazohusika.