NA DIRAMAKINI
BENKI Kuu ya Tanzania imeshiriki katika Soko la jumla la Fedha za Kigeni (IFEM) kwa mujibu wa
Sera yake ya ushiriki katika soko la Fedha za Kigeni ya mwaka 2023.
Katika ushiriki huo, Benki
Kuu imeuza Dola za Marekani milioni 30.25 kupitia mnada wa ushindani kwa kiwango cha wastani
cha kubadilisha fedha za kigeni cha Shillingi 2,469.96 kwa Dola moja ya Marekani. Lengo la mnada
huu lilikuwa ni kuongeza ukwasi katika soko la fedha za kigeni.

