RABAT-Rais wa Shirikisho la Kandanda Duniani (FIFA),Bw. Gianni Infantino amesema, FIFA ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika programu zake za maendeleo ambazo zitasaidia kutengeneza fursa kwa vijana kunufaika na mchezo wa mpira wa miguu ikiwemo ujenzi wa miundombinu na uendelezaji wa vituo vya ufundi.
Infantino amezungumza hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Paul Makonda na ujumbe wake kando ya tukio la mechi ya fainali ya michuano ya michuano ya AFCON 2025 iliyofanyika jijini, Rabat Morocco.
Infantino ameipongeza Tanzania kwa kazi kubwa iliyofanywa na inayoendelea kufanywa na Serikali ya ujenzi wa miundombinu ya michezo kuelekea AFCON 2027 na amesema FIFA itaunga mkono jitihada hizo.
Kwa upande wake Waziri Makonda amemshukuru Bw. Infantino kwa ushirikiano mkubwa anaoutoa kwa Tanzania katika maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu na amemhakikishia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali anayoiongoza inaunga mkono jitihada hizo na ipo tayari kushirikiana na FIFA.Mheshimiwa Makonda amemkaribisha Tanzania Bw. Infantino na amemwambia Tanzania ipo tayari kuwa mwenyeji wa matukio mbalimbali ya FIFA ikiwemo mashindano mbalimbali, mikutano na ziara za viongozi na wataalamu.
Halikadhalika Bw. Makonda amemualika Bw. Infantino kuja Tanzania kuangalia maandalizi ya kuelekea uenyeji wa AFCON.
Halikadhalika Bw. Makonda amemualika Bw. Infantino kuja Tanzania kuangalia maandalizi ya kuelekea uenyeji wa AFCON.
