Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, ACP Almachius Mchunguzi, akipata maelezo kutoka kwa Mwanasheria wa Bodi ya Bima ya Amana (DIB), Bi. Esther Mpendaamani kuhusu majukumu ya DIB wakati alipotembelea banda la DIB katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya Usagara jijini Tanga tarehe 21 Januari 2026.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, ACP Almachius Mchunguzi, akielezea kufurahishwa na maelezo kuhusu majukumu ya DIB na namna taasisi hiyo inavyowaelimisha wananchi jinsi inavyokinga amana zao katika benki na taasisi za fedha wakati alipotembelea banda la Bodi ya Bima ya Amana katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya Usagara jijini Tanga.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Umma na Mawasiliano wa DIB, Lwaga Mwambande akifafanua jambo kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, ACP Almachius Mchunguzi.







