Magazeti leo Januari 13,2026

Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha mwaka 2026 imejenga na kufungua shule mpya za awali na msingi za mchepuo wa Kiingereza, hatua inayolenga kukidhi mahitaji ya wananchi waliokuwa wakihitaji huduma hiyo kwa gharama nafuu.
Miongoni mwa shule hizo ni Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere iliyopo Kata ya Sofu, ambayo tayari imekamilika kwa gharama ya sh. Milioni 569,264,013.76 kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri, ikiwa na madarasa ya kisasa, madawati, vyoo na walimu wa kutosha.

Aidha, Shule ya Msingi Mwambisi iliyopo Kata ya Kongowe ipo katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa ujenzi ambapo hadi sasa, jumla ya sh. Milioni 252,897,072.40 tayari zimekwishatolewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo, huku milioni 151,760,000.00 zikitarajiwa kutolewa ili kukamilisha ujenzi wake.

Akizungumza kuhusu miradi hiyo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha Dkt. Shemwelekwa alisema uanzishwaji wa shule hizo ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha watoto wanapata elimu bora katika mazingira rafiki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here