BoT yatoa elimu kwa wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini

DAR-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa elimu kwa wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini kuhusu majukumu yake ya msingi katika kusimamia na kuimarisha uchumi wa taifa, ikiwemo usimamizi wa sekta ya fedha na juhudi za kukuza ubunifu katika huduma za kifedha.
Elimu hiyo imetolewa Januari 15,2026, wakati wanafunzi zaidi ya 200 kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro (MUM) na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) walipofanya ziara ya mafunzo katika ofisi za Benki Kuu jijini Dar es Salaam.
Kupitia ziara hiyo, wanafunzi walipata fursa ya kujifunza kuhusu majukumu ya msingi ya Benki Kuu katika kusimamia sera za fedha na kulinda thamani ya shilingi ya Tanzania, usimamizi na uangalizi wa taasisi za kifedha nchini, uwezeshaji wa upatikanaji wa huduma za kifedha zinazozingatia misingi ya Sharia (Islamic Banking), pamoja na ubunifu na mageuzi yanayoendelea katika sekta ya fedha kwa lengo la kuongeza ufanisi na ujumuishwaji wa kifedha.

Wanafunzi walieleza kufurahishwa na fursa hiyo ya kupata elimu moja kwa moja kutoka kwa wataalamu wa BoT, wakisema kuwa mafunzo hayo yamewaongezea uelewa mpana kuhusu masuala ya uchumi na sekta ya fedha, pamoja na kuwajengea hamasa ya kuyafuatilia kwa kina zaidi.
Ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za Benki Kuu katika kuimarisha utoaji wa elimu kwa umma, hasa kwa vijana wanaojifunza taaluma za uchumi na fedha, kwa nia ya kuandaa rasilimali watu yenye maarifa ya kutosha kuhusu mifumo ya kifedha na nafasi yake katika kuchochea maendeleo ya taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here