Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 imekutana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla, na kusikiliza taarifa mbalimbali kuhusu matukio hayo.
Mazungumzo hayo yamefanyika Januari 5,2026 katika ukumbi wa Ngorongoro TourismCenter Mkoani Arusha. Katika kikao hicho miongoni mwa mambo waliojadili ni namna matukio hayo yalivyoanza, athari zake kwa wakazi wa Mkoa wa Arusha, pamoja na uharibifu wa mali na miundombinu.
Tume bado inaendelea kukusanya taarifa mbalimbali kwa waathirika wa matukio ya uvunjifu wa amani ziliztokea Oktoba 29 Uchaguzi Mkuu katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar-es-salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya. 

Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo























