Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar afungua Maonesho ya 12 ya Kimataifa ya Biashara ya Zanzibar

ZANZIBAR-Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla amefungua rasmi Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 62 ya Zanzibar yanayoendelea katika viunga vya maonesho vya Nyamanzi, Fumba mjini Unguja.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo, Makamu wa Pili wa Rais Mheshimiwa Abdulla amesisitiza umuhimu wa maonesho hayo kama chombo cha kukuza biashara, kuongeza fursa za uwekezaji na kuinua sekta ya uzalishaji hasa kwa wajasiriamali wa ndani.

Alieleza kuwa serikali itaendelea kuwa miongoni mwa waungaji mkono wakuu wa biashara ndogo ndogo, za kati na kubwa ili kuhakikisha ukuaji endelevu wa uchumi wa visiwa vya Zanzibar na Pemba.
Mheshimiwa Abdulla ametembelea mabanda mbalimbali yanayoshiriki katika maonesho hayo ikiwa ni pamoja na banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Taasisi zake za AICC,APRM na Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt.Salim Ahmed Salim.

Katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Abdullah Abdullah alipokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Afisi ya Mambo ya Nje Zanzibar Bw. Ally Ally na wafanyakazi wa Wizara walioko katika afisi hiyo.

Mheshimiwa Abdulla amewapongeza watumishi wa Wizara na taasisi zake kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya katika kutekeleza majukumu yao.
Naye Mkurugenzi wa Maonyesho hayo amewataka wadau walioshiriki maonesho hayo kutumia fursa hiyo ya kipekee kuuza bidhaa, kutafuta washirika wa kibiashara na kupanua mitandao ya uwekezaji kwa kuwa maonyesho hayo ni jukwaa muhimu la kukuza soko la ndani na nje ya nchi.

Maonesho hayo yanashirikisha zaidi ya taasisi 316 kutoka serikalini, kampuni binafsi na washirika wa kimataifa yatamalizika Januari 16,2026.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here