Rais Dkt.Samia afanya uteuzi na utenguzi wa viongozi mbalimbali

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na utenguzi wa viongozi mbalimbali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 8,2026 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt.Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa na kutenguliwa ni Mhe. Patrobas Paschal Katambi (Mb.) ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kabla ya uteuzi huo, Mhe. Katambi alikuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,ambapo anachukua nafasi ya Mhe. Boniface George Simbachawene (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Pia, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Mhe.Prof. Palamagamba John Aidan Kabudi (Mb.) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum). Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Prof. Kabudi alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Aidha,Mhe. Paul Christian Makonda (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Makonda alikuwa Naibu Waziri katika wiz0ara hiyo.

Katika hatua nyingine,Mhe. Dennis Lazaro Londo (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara. Kabla ya uteuzi huo, Mhe. Londo alikuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi;

Mheshimiwa Rais Dkt.Samia pia amemteua, Mhe. Ayoub Mohamed Mahmoud (Mb.) kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Dkt.Richard Stanslaus Muyungi ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira). Dkt. Muyungi anachukua nafasi ya Mhandisi Cyprian John Luhemeja ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

Wengine walioteuliwa na Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ni Mhandisi Zena Ahmed Said kuwa Balozi,Bw. Waziri Rajab Salum ameteuliwa kuwa Balozi na Meja Jenerali Mbaraka Naziad Mkeremy ameteuliwa kuwa Balozi.

Naye Mhandisi Ally Samaje ameteuliwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST). Mhandisi Samaje anachukua nafasi ya Dkt. Mussa Daniel Budeba.

Ris Dkt.Samia, pia ametengua uteuzi wa Prof. Eliakimu Mnkondo Zahabu, Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,uapisho wa viongozi wateule utafanyika Januari 13,2026 katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma kuanzia saa 8.00 mchana.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here