ZANZIBAR-Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, amezindua rasmi Maonesho ya 12 ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar (ZITF) katika viwanja vya Nyamanzi Januari 7, 2026.
Ameeleza kuwa, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji na wafanyabiashara, huku akisisitiza umuhimu wa sekta binafsi katika kufanikisha maendeleo endelevu ya taifa.
Katika hafla hiyo, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) iliwakilishwa na Mkurugenzi wa TMA ofisi ya Zanzibar, Masoud Makame Faki, ambaye aliwakumbusha wananchi kutembelea banda la TMA ili kupata elimu ya sayansi ya hali ya hewa, hususan katika kipindi hichi ambacho dunia inakabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi, ambapo mifumo ya hali ya hewa imekuwa ikibadilika mara kwa mara na kusababisha athari kwa sekta mbali mbali za uchumi na kijamii.
Hivyo basi matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa ni suluhisho mbadala kwa ajili ya kukuza uchumi na biashara katika sekta tofauti zikiwemo kilimo, uvuvi, viwanda, nishati, ujenzi, mawasiliano nakadhalika.
Tags
Habari
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)
Tanzania Meteorological Agency (TMA)
Utabiri wa Hali ya Hewa Tanzania

