Polisi Mwanza wafanya sherehe ya kuukaribisha Mwaka Mpya 2026

MWANZA-Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza leo Januari 10,2026 limefanya sherehe kwa askari na familia zao kuukaribisha mwaka mpya 2026 kwa lengo la kuimarisha uhusiano na mashirikiano ili kuweza kufanya kazi kwa weledi wakiwa na furaha.
Sherehe hiyo pia ilihudhuriwa na Maofisa, Wakaguzi, Askari wa vyeo mbalimbali ndungu wa karibu pamoja na familia za askari katika viwanja vya Polisi Mabatini Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza na kufuatiwa na michezo pamoja na burudani mbalimbali.
Sherehe ya kuukaribisha Mwaka Mpya 2026 Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limekuwa na utaratibu wa kusheherekea kwa pamoja askari na familia zao ili kubadilishana mawazo na kujiwekea mikakati kwa mwaka mpya ili kukuza ustawi wa familia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here