NA DIRAMAKINI
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemteua Profesa Hamed R. H. Hikmany kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 19,2025 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi Zena A. Said, ikieleza kuwa uteuzi huo umeanza leo.

