Serikali inaendelea kuimarisha mazingira bora ya uwekezaji Zanzibar-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewahakikishia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwa Serikali itaendelea kuweka vivutio na mazingira bora ya uwekezaji kwa lengo la kunufaika na miradi yao.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Januari 20,2026, wakati wa uzinduzi wa boti mpya ya Kilimanjaro 9 (Dragon of the Sea) inayomilikiwa na Kampuni ya Azam Marine Ltd, katika hafla iliyofanyika Mtoni Verde, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Amesema, Serikali inaendelea kuimarisha sekta ya usafirishaji baharini kupitia ujenzi wa miundombinu ya bandari ikiwemo Bandari ya Fumba na bandari nyingine Unguja na Pemba, hatua itakayochochea ukuaji wa uchumi na kuboresha huduma za usafiri baharini.

Rais Dkt. Mwinyi amempongeza Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam, Mzee Said Salim Bakhresa, kwa uwekezaji mkubwa unaogusa maisha ya wananchi, akibainisha kuwa kampuni hiyo imewekeza Dola za Marekani Milioni 150 na kutoa ajira 281.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Azam, Ndg. Aboubakar Azizi, amesema boti hiyo iliyotengenezwa China ina uwezo wa kubeba abiria 631 na ina mifumo ya kisasa ya kulinda mazingira ya bahari.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA, Ndg. Saleh Saad Muhammed, amesema hadi sasa miradi ya uwekezaji yenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 6.8 imesajiliwa, ikitoa ajira 28,000 za moja kwa moja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here