NA DIRAMAKINI
KATIKA safari ya maisha, binadamu mara nyingi husahau jambo moja la msingi, kwamba muda hauchelewi kwa mtu yeyote.
Kadri siku zinavyopita, umri husonga mbele bila kusita, na kila hatua ya maisha hubeba wajibu, tafakari na maandalizi ya mustakabali wa mwisho wa mwanadamu.
Kwa mtazamo wa kijamii na kimaadili, maisha ya binadamu yanaweza kugawanywa katika hatua mbalimbali za umri, kuanzia utoto, ujana, utu uzima hadi uzee wa mwisho. Kila kundi la umri lina changamoto, fursa na wajibu wake.
Hatua za juu za umri, kuanzia miaka ya tisini na kuendelea, hufananishwa na machweo ya maisha, ambako binadamu hutakiwa kuangalia nyuma na kutathmini safari yake.
Umri wa kati, kuanzia miaka ya arobaini hadi sitini, ni kipindi cha maamuzi, mafanikio na marekebisho, wakati ambapo athari za maamuzi ya awali huanza kuonekana wazi.
Aidha,umri wa ujana na makuzi, kwa upande mwingine, ni msingi wa kujenga ndoto, maadili na mwelekeo wa maisha. Tazama mtiririko ufuatavyo;
1:Umri wa Ziada
1926 – Miaka 100
1927 – Miaka 99
1928 – Miaka 98
1929 – Miaka 97
1930 – Miaka 96
1931 – Miaka 95
1932 – Miaka 94
2:Umri wa Machweo
1933 – Miaka 93
1934 – Miaka 92
1935 – Miaka 91
1936 – Miaka 90
1937 – Miaka 89
1938 – Miaka 88
1939 – Miaka 87
1940 – Miaka 86
1941 – Miaka 85
1942 – Miaka 84
1943 – Miaka 83
1944 – Miaka 82
1945 – Miaka 81
1946 – Miaka 80
1947 – Miaka 79
1948 – Miaka 78
1949 – Miaka 77
1950 – Miaka 76
1951 – Miaka 75
3:Uzee
1952 – Miaka 74
1953 – Miaka 73
1954 – Miaka 72
1955 – Miaka 71
1956 – Miaka 70
1957 – Miaka 69
1958 – Miaka 68
1959 – Miaka 67
1960 – Miaka 66
1961 – Miaka 65
1962 – Miaka 64
1963 – Miaka 63
4:Umri wa Marekebisho na Maridhiano
1964 – Miaka 62
1965 – Miaka 61
1966 – Miaka 60
1967 – Miaka 59
1968 – Miaka 58
1969 – Miaka 57
1970 – Miaka 56
1971 – Miaka 55
1972 – Miaka 54
1973 – Miaka 53
5:Umri wa Mafanikio na Utimilifu
1974 – Miaka 52
1975 – Miaka 51
1976 – Miaka 50
1977 – Miaka 49
1978 – Miaka 48
1979 – Miaka 47
1980 – Miaka 46
1981 – Miaka 45
1982 – Miaka 44
1983 – Miaka 43
6:Umri wa Kufanya Maamuzi
1984 – Miaka 42
1985 – Miaka 41
1986 – Miaka 40
1987 – Miaka 39
1988 – Miaka 38
1989 – Miaka 37
1990 – Miaka 36
1991 – Miaka 35
1992 – Miaka 34
1993 – Miaka 33
7:Umri wa Kujitoa na Dhamira
1994 – Miaka 32
1995 – Miaka 31
1996 – Miaka 30
1997 – Miaka 29
1998 – Miaka 28
1999 – Miaka 27
2000 – Miaka 26
2001 – Miaka 25
2002 – Miaka 24
2003 – Miaka 23
8:Umri wa Ujana na Masomo
2004 – Miaka 22
2005 – Miaka 21
2006 – Miaka 20
2007 – Miaka 19
2008 – Miaka 18
2009 – Miaka 17
2010 – Miaka 16
2011 – Miaka 15
2012 – Miaka 14
2013 – Miaka 13
9:Umri wa Uangalizi wa Watoto Wachanga na Wadogo
2014 – Miaka 12
2015 – Miaka 11
2016 – Miaka 10
2017 – Miaka 9
2018 – Miaka 8
2019 – Miaka 7
2020 – Miaka 6
2021 – Miaka 5
2022 – Miaka 4
2023 – Miaka 3
2024 – Miaka 2
2025 – Mwaka 1
Hata hivyo, ujumbe mkubwa unabaki kuwa mmoja kwamba,hakuna aliye mdogo wala mkubwa kiasi cha kupuuza wajibu wa maisha.
Jamii inakumbushwa kuepuka kujidanganya kuwa bado kuna muda mwingi wa kufanya yaliyo sahihi.
Kila siku inayopita humsogeza binadamu karibu na mwisho wake. Ni vyema kila mmoja ajiulize; Nimefanya nini cha maana kwa familia yangu, jamii na kwa Mungu?.
Je, mchango wangu unaacha alama gani kwa wengine?. Nifanye nini leo kabla ya kuchelewa?.
Kumbuka
Siku moja mtu atastaafu, siku moja nafasi yake itachukuliwa na mwingine, siku moja mali na hadhi vitapoteza maana.
Siku moja jina lake litatanguliwa na neno marehemu, na siku moja atasimama mbele ya Muumba wake kutoa hesabu ya matendo yake.
Hakuna cheo, mali, uzoefu wala umaarufu vitakavyosalia. Kitakachobaki ni matendo mema au mabaya.
Tuishi kwa unyenyekevu, kufanya mema, kuepuka uovu na kuishi kwa amani na watu wote.
Pia, ishi kwa kumpenda jirani, acha dhuluma, kuthamini maisha, na kumweka Muumba mbele ya mambo ya dunia.
Kwa hakika, dunia ni ya kupita, lakini athari ya matendo ya mtu ni ya kudumu.Binadamu hukumbukwa si kwa alichomiliki, bali kwa yale aliyoyatenda.
