Ufaulu wa Mitihani ya Kidato cha Nne 2025 waongezeka nchini, NECTA yatangaza matokeo

NA DIRAMAKINI

BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza rasmi matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) wa mwaka 2025, uliofanyika kuanzia tarehe 17 Novemba hadi 5 Desemba 2025, huku takwimu zikionesha ongezeko la ufaulu ikilinganishwa na mwaka 2024.
Akizungumza leo Januari 31,2026 na waandishi wa habari baada ya mkutano wa Baraza la 170 uliofanyika tarehe 26 Januari 2026, Katibu Mtendaji wa NECTA, Profesa Said Mohamed amesema, jumla ya watahiniwa 595,810 walisajiliwa kufanya mtihani huo, wakiwemo Wasichana 318,910 (asilimia 53.53) na Wavulana 276,900 (asilimia 46.47).

Kati yao, watahiniwa wa shule walikuwa 569,883, huku watahiniwa wa kujitegemea wakiwa 25,927.

Kwa upande wa watahiniwa wa shule, jumla ya 555,606 (asilimia 97.49) walifanya mtihani, ambapo Wasichana 295,554 (asilimia 97.27) na Wavulana 260,052 (asilimia 97.76) walihudhuria. Watahiniwa 14,277 (asilimia 2.51) hawakufanya mtihani.

Kwa watahiniwa wa kujitegemea, 22,794 (asilimia 87.92) walifanya mtihani, huku 3,133 (asilimia 12.08) wakikosa.

Matokeo yanaonesha kuwa watahiniwa wa shule 526,620 (asilimia 94.98) wamefaulu kwa kupata madaraja ya I hadi IV, ikilinganishwa na asilimia 92.37 mwaka 2024. Hii ni ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2.61.

Katika ufaulu huo, Wasichana 278,108 (asilimia 94.26) walifaulu, huku Wavulana 248,512 (asilimia 95.79) wakifaulu.

Kwa watahiniwa wa kujitegemea, 16,794 (asilimia 73.83) walifaulu, ikilinganishwa na asilimia 62.51 mwaka 2024, sawa na ongezeko la asilimia 11.32.

NECTA imeeleza kuwa ubora wa ufaulu pia umeimarika, ambapo watahiniwa wa shule 255,404 (asilimia 46.06) walipata madaraja ya I hadi III, ikilinganishwa na asilimia 42.96 mwaka 2024. Ongezeko hilo ni la asilimia 3.10.

Takwimu zinaonesha kuwa, wavulana walifanya vizuri zaidi katika madaraja ya juu (I–III) kwa asilimia 52.30, ikilinganishwa na wasichana asilimia 40.58.

Kati ya shule 5,843 zilizoshiriki, shule 5,839 (asilimia 99.93) zilipata wastani wa daraja A hadi D. Aidha, shule zilizopata wastani wa daraja A hadi C zimeongezeka kutoka 2,494 (asilimia 44.83) mwaka 2024 hadi 2,935 (asilimia 50.23) mwaka 2025, sawa na ongezeko la asilimia 5.40.Tazama matokeo yote hapa

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here