Waziri Balozi Kombo afanya mazungumzo na Balozi wa Burundi nchini Tanzania

DODOMA-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amefanya mazungumzo na Balozi wa Burundi, Mhe. Leontine Nzeyimana jijini Dodoma Januari 14, 2026.
Viongozi hao walisisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa karibu kati ya Tanzania na Burundi kwa madhumuni sio tu ya kuimarisha zaidi uhusiano wa kindugu uliopo baina ya nchi hizo, bali pia kusimamia utekelezaji wa miradi ya pamoja ikiwemo ya miundombinu ambayo inalenga kuzifungua nchi hizo kiuchumi kwa manufaa ya wananchi wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here