Kuelekea maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha

TANGA-Kikao cha Uratibu wa Maandalizi ya Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha kimefanyika jijini Tanga kikihusisha Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa wa Tanga.
Lengo la kikao hicho ni kuweka mikakati na maandalizi ya pamoja kuelekea maadhimisho hayo muhimu kwa maendeleo ya wananachi.

Kikao hicho kilihudhuriwa na wawakilishi wa makundi mbalimbali yakiwemo; Wanawake na Samia, Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake, Kikundi cha Wajane, Tanga Women Galla, Wafanyabiashara wadogowadogo pamoja na Viongozi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na jiji la Tanga.

Aidha, wajumbe wote wameazimia kuwa kila Kiongozi wa kikundi, Mtumishi, na Wadau wote wawe mabalozi wazuri kuhakikisha kuwa wanahamasisha wananchi wa mkoa wa Tanga na mikoa ya jirani kushiriki kwa wingi ili kupata Elimu ya Fedha ambayo itatolewa bila malipo yeyote itakayoboresha maisha yao.

Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha yanatarajiwa kuanza tarehe 19 hadi 26 Januari, 2026 katika viwanja vya Usagara jijini Tanga, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb). Lengo ni kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu huduma za fedha na fursa za kiuchumi zilizopo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here