Askari wa kike wafundwa

DAR-Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kariakoo Mrakibu wa Polisi,SP Eugene Mwampondele ambaye pia ni mlezi wa Mtandao wa wanawake wilaya ya Kariakoo, amewataka askari wa kike kutumia fursa mbalimbali wanazozipata ili kujiimarisha kiuchumi.
SP Eugene ameyasema hayo Februari 06, 2026 wakati akiongea na askari wanachama wa Mtandao wa Polisi wanawake wilaya ya Kariakoo katika Ukumbi wa mikutano wa Cate Hotel iliyopo Mtaa wa Swahili Kariakoo,Dar es Salaam.
“Tambueni fursa zilizopo sambamba na kujadili kwa pamoja changamoto zinazowakabili kama familia na kuzitafutia ufumbuzi. Nimefurahi kuona leo hii mko hapa mmeitana ili kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata somo la ujasiriamali,” amesema SP Eugene.
Kauli hiyo imeungwa mkono na Bi. Joyce Mwalukasa ambaye ni mjasiriamali na mfanyabiashara mbalimbali hapa Dar es Salaam, ambapo amewahimiza askari wa kike kutokukata tamaa wanapokutana na changamoto katika utafutaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here