Rais Museveni awasili nchini kwa ziara ya kikazi

DAR-Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni amewasili jijini Dar es Salaam, Tanzania, kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Mara baada ya kuwasili, Rais Museveni atafanya mazungumzo ya pande mbili na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, mazungumzo hayo pamoja na masuala mengine yatalenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kukuza ushirikiano sekta muhimu za uchumi ikiwemo nishati kati ya Tanzania na Uganda,hususan Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).
Vilevile wataangazia masuala ya kikanda na kimataifa yenye maslahi ya pamoja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here